- 1,171 viewsAliyekuwa mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC), Wafula Wanyonyi Chebukati, aliaga dunia jana Alhamisi katika hospitali moja mjini Nairobi akiwa na umri wa miaka 63, baada ya kuugua kwa muda mrefu, kama ilivyothibitishwa na familia yake. Chebukati aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa IEBC mwaka 2017 na Rais wa wakati huo Uhuru Kenyatta. Kipindi chake kama mwenyekiti wa tume hiyo kilikumbwa na changamoto nyingi zikiwemo za kusimamia chaguzi za mwaka 2017 na 2022 zilizoghubikwa na utata. Matokeo ya uchaguzi wa urais wa 2017 yalibatilishwa na Mahakama ya Juu kwa sababu ya kasoro, na kusababisha uchaguzi wa marudio. Katika uchaguzi wa 2022, Chebukati alimtangaza William Ruto kama Rais mteule, akimshinda mpinzani wake wa karibu, Raila Odinga, huku kukiwa na mgawanyiko ndani ya tume hiyo. Makamishna wanne walipinga matokeo hayo na kusababisha mtafaruku mkubwa wa kisisa katika taifa hilio la Afrika Mashariki. Licha ya mzozo wa ndani na shinikizo kutoka nje, Chebukati aliendelea kutetea matokeo yaliyotangazwa, ambayo baadaye yaliidhinishwa na Mahakama ya Juu. Kipindi chake pia kilikumbwa na matukio ya kusikitisha, ikiwa ni pamoja na vifo vya maafisa wa IEBC Chris Msando 2017 na Daniel Musyoka 2022. Rais William Ruto aliomboleza kifo cha Chebukati akimtaja kuwa kiongozi aliyetumikia taifa kwa uadilifu, akisema kuwa kifo chake ni hasara kubwa kwa taifa. Chebukati ameacha mjane Mary Chebukati Wanyonyi, ambaye aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Ugavi wa Mapato 2023, na watoto kadhaa. - VOA Swahili #IEBC #WafulaWanyonyiChebukati #kifo #maombolezi #Rais #kenya #williamruto
Mwenyekiti wa zamani wa IEBC afariki akiwa na umri wa miaka 63
- 26 Jun 2025 - Shabiki, through its Na Jamii corporate social responsibility initiative, proudly sponsored the KidsToKids Charity Golf Tournament, a one-of-a-kind event that raised funds to support education for underprivileged children in Kenya.
- 26 Jun 2025 - Some 26 Nyandarua County government vehicles were torched during Wednesday’s demonstrations to mark the first anniversary of last year’s anti-Finance Bill protests.
- 26 Jun 2025 - Iran's intelligence services have arrested 26 people, accusing them of collaborating with Israel, state media Fars news agency reported, days after a ceasefire between the two countries was announced.
- 26 Jun 2025 - Sixteen people died during nationwide anti-government protests in Kenya on Wednesday, most of them killed by police, the head of Amnesty Kenya said, a year after deadly demonstrations against a tax bill culminated in the storming of parliament.
- 26 Jun 2025 - Ecuador's president announced Wednesday that the country's most-wanted fugitive, Los Choneros gang leader "Fito," had been recaptured over a year after his escape from prison triggered a wave of violence.
- 26 Jun 2025 - Kalonzo said he understands the frustration and grief felt by the youth.
- 26 Jun 2025 - Lobby groups said at least eight people were killed and 400 injured in the protests.
- 26 Jun 2025 - In a statement on X, Kaluma said the CA’s move was in the interest of public safety and order.
- 26 Jun 2025 - Protesters barricaded roads, lit bonfires, and engaged police in fierce confrontations
- 26 Jun 2025 - Live coverage of peaceful demonstrations is not incitement to violence.