Wakenya waandamana kulalamikia kifo cha mwanablogu Ojwang

  • | BBC Swahili
    6,725 views
    Kumekuwa na maandamano ya wanaharakati jijini Nairobi hii leo kufuatia kifo cha mwanablogu na mwalimu Albert Omondi Ojwang, ambaye aliaga dunia akiwa kizuizini katika kituo cha polisi cha Central Nairobi. Polisi wanasema Albert alifariki kutokana na majeraha ya kichwa akiwa kizuizini, na kwamba alijisababishia majeraha hayo mwenyewe.