- 852 viewsRais wa Kenya William Ruto Ijumaa alimteua waziri wa mambo ya ndani Kithure Kindiki kuwa naibu wake mpya, siku moja baada ya baraza la Seneti kupiga kura ya kumtimua naibu wake wa zamani, Rigathi Gachagua. “Nimepokea ujumbe kutoka kwa rais, kuhusu kuteuliwa kwa Profesa Kithure Kindiki kushika nafasi hiyo ambayo imetokea afisini,” Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula alisema Ijumaa, akiwahutubia wabunge mjini Nairobi. Gachagua, ambaye alikanusha mashtaka yote dhidi yake wakati wa kesi ya kuondolewa madarakani, alimuunga mkono Ruto katika ushindi wake wa 2022 na kusaidia kupatikana kwa kura nyingi kutoka eneo lenye wakazi wengi la kati mwa Kenya. Lakini katika miezi ya hivi karibuni , Gachagua amezungumza kuhusu kutengwa, huku kukiwa na taarifa zilizoenea kwenye vyombo vya habari kuwa ametofautiana na Ruto wakati miungano ya kisiasa ikibadilika. Kindiki, mshirika wa karibu wa Ruto, ameshikilia wadhifa wa wizara ya mambo ya ndani katika kipindi chote cha miaka miwili ya Ruto kama rais. Hapo awali aliwahi kuwa seneta wa Kaunti ya Tharaka Nithi na alikuwa mgombeaji mkuu kuwa mgombea mwenza wa Ruto wakati wa uchaguzi wa 2022. Baadaye Bunge litalazimika kupiga kura kuidhinisha uteuzi wa Kindiki kabla ya kuapishwa. #Kenya #seneti #gachagua #kindiki #voa #voaswahili
'Nawaunga mkono wabunge na seneti kwa muelekeo wao...'
- 26 Jun 2025 - Interior Cabinet Secretary Kipchumba Murkomen has vehemently castigated the Wednesday, June 25, demonstrations, citing that the protesters had a motive to forcefully seize power through a coup.
- 26 Jun 2025 - In a statement released Thursday, the country's leading legal body expressed condolences to the families of the eight people confirmed to have died during the nationwide protests, one year after the 2024 anti-Finance Bill demonstrations.
- 26 Jun 2025 - The Kenya Union of Journalists (KUJ), Kenya Editors Guild (KEG), Association of Media Women in Kenya (AMWIK), and Kenya Correspondents Association have filed a petition in the High Court claiming that the government's actions violate several fundamental…
- 26 Jun 2025 - The decision targets Kenyans who are living in the United States.
- 26 Jun 2025 - Several police stations were infiltrated and destroyed.
- 26 Jun 2025 - Speaking a day after the nationwide demonstrations, Kimilili MP Didmus Barasa criticized court-imposed restrictions on police use of force, claiming they left officers powerless in the face of unrest.
- 26 Jun 2025 - The court has since been closed indefinitely.
- 26 Jun 2025 - They are accused of inciting the youth.
- 26 Jun 2025 - The defence maintained that the real owner of the account in question is missing.
- 26 Jun 2025 - "They are mobilising people to participate."